England yamuingiza Kane katika ugomvi wa Messi na Christian Ronaldo

England imeanza harakati za kutaka kumpaisha Harry Kane mchezaji wa Spurs ambae pia ni raia wa chini humo ili aweze kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2014/15 katika vita ambayo kwa miaka nane mfululizo imekuwa ni vita ya Messi na CR7 ambao wachezaji hao wameonekana kuwa bora zaidi na kusemekana ni wa sayari nyingine lakini England wanahitaji Kane achukue tuzo hiyo ambayo hucheza katika mikono ya waliobora zaidi Kane kwa sasa anaongoza katika orodha ya wafungaji katika ligue hiyo ya nchini kwao akifungana na Diego Costa wa Chelsea wote wakiwa na magoli 19 lakini nyuma yuko yule aliezoeleka kukimbiza kijiti cha magoli Sergio Khun Agüero wa Manchester city ambae ana magoli 17 akifuatiwa na kijana anaekuja mbio katika ufungaji Charlie Austin wa QPR mwenye magoli 15 Kwa ligi ya EPL ni ligi maarufu sana ambao umaarufu huo unatokana na lugha wanayoitumia lakini pia kujitangaza zaidi na kutoa nafasi za wawekezaji zaidi na mara kadhaa England wamekuwa ni watu wa kujali utaifa wao...