Christian Ronaldo ampiku Leo Messi Gareth Bale baba lao
Wakaa wanasoka ikiendelea kupamba moto kwa mpambano baina ya washambuliaji wawili wa timu hasimu nchini Hispania Barcelona na Real madrid ambao ni baina ya Leo Messi na Christiano Rinaldo ambapo kila siku zimekuwa zikitoka takwimu za kuwalinganisha hawa jamaa wawili na kutafuta ni nani bora zaidi ya mwingine mpambano huu unaendelea ambapo mtandao wa LIGA Bancomer MX umetoa takwimu zinazoonyesha mchezaji mwenye kasi zaidi ulimwenguni wakati anapokokota mpira. Takwimu hiyo inawahainisha wachezaji kumi bora pekee ambao wameonekana kuwa wenye kasi zaidi wanapo kokota mipira wakati wakishambulia ambapo winga Gareth Bale wa Real Madrid ameshika namba moja kwa kukokota kwa kasi ya kilomita 36.9 kwa saa na kuwa kinara. Wakati Christian Ronaldo akimpiku hasimu wake kwa kushika nafasi ya tano huku akiwa na kasi ya kilomita 33.6 kwa saa akiwa kampita mpinzani wake kwa kasi ya kilomita 1.1 kwa saa, Leo Messi ameshika nafasi ya saba nyuma ya Theo Walcott mwenye kasi ya kilomita 32.7 kwa saa aliyemuacha kwa kasi ya kilomita 0.1 kwa saa kwa takwimu hizi zinaonyesha Ubora wa Ronaldo wa kukimbiza mipira zaidi wakati wa kulisogelea lango la team pinzani huku akimuacha Messi mwenye aina tofauti kidogo anaposhika mpira hukimbiza huku akitafuta kutengeneza nafasi ya kutoa pasi maridadi kwa wanaomzunguka. Kwa leo Christian Ronaldo ameonekana kung'aa zaidi ya Messi katika kasi lakini Bale ndo habari ya mjiniwww.facebook.com
Comments
Post a Comment