EPL yawaka moto Ronaldo akunja ngumi
Katika wiki kadhaa ligi nyingi ulaya zilikuwa zimesimama na badala yake kulikuwa na mashindano katika timu za taifa na pia ni mechi za kirafiki Lakini kutokana na kiu ya muda mrefu kwa mashabiki wa ligi za ulaya sasa ilirejea katika mwisho wa juma lilopita Jumamosi kulikuwa na baadhi ya mechi kali zilizokutanisha timu kadhaa kubwa ambako moja kati ya mechi kali iliyokuwa ikisubiriwa na wengi ni mechi baina ya Arsenal na Liverpool mechi ambayo arsenal walikuwa nyumbani emirates ambako jumamosi hiyo walijichinjia jogoo lao la pasaka na kuliweka kwenye jokofu kwa ajili ya pasaka, Arsenal iliicharaza Liverpool kwa idadi ya magoli 4 kwa 1 ambapo magoli hayo yalifungwa na Bellerin dakika ya 37 akipokea pasi safi kutoka kwa Ramsey na dakika ya 40 ya mchezo mjerumani M. Ozil alipiga faulo safi aliyozama wavuni ambayo bila shaka ni faulo bora tangu aanze kukipga arsenal na Ramsey hakuchoka kutengeneza magoli alimkatia pande maridadi Sanchez ambae alipiga muwa uliozama wavuni na kuandik...