Messi amburuza Ronaldo huku Alexis Sanchez kumipiku Hazard katika tuzo za msimu
Wakati Leo Messi akitangazwa kuwa ni mchezaji bora wa mwaka katika ligi ya Uhispania kwa kunyakua asilimia 55.87 dhidi ya 35.37 asilimia alilozipata hasimu wake Cristiano Ronaldo ambapo Messi alionekana kuwa bora zaidi ya Ronaldo mara baada ya kuiwezesha timu yake kunyakuwa ubingwa wa ligi ya hispania kwa kuifungia magoli muhimu na kutengeneza magoli mawili zaidi ya hasimu wake ambae alionekana kuwa vizuri zaidi katika ufungaji msimu huu huku akiwa tayari amefunga msimu kwa kufunga magoli 61 dhidi ya 56 ya Messi ambae amebakiwa na mechi mbili mkononi. Upande wa pili mchezaji hatari wa zamani katika timu ya Barcelona ambae kwa sasa anakipiga katika klabu ya Arsenal Alexis Sanchez ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya mashabiki ya PFA kwa msimu huu akimpiku Hazard wa Chelsea na Sergio Kun Aguero na mlinda mlango David de Gea
Comments
Post a Comment