LIONEL MESSI NI MCHEZAJI BORA WA MUDA WOTE
Kocha wa zamani wa klabu ya Barca PEP GUARDIOLA ameibuka na kusema kuwa Messi ni mchezaji bora wa muda wote akionekana kumfananisha na mchezaji mkongwe wa Brazil PELE. PEP aliyasema hayo jana baada ya kuishuhudia Barca ikikiondoa kikosi chake cha Bayern munich katika michuano ya ulaya kwa jumla ya magoli matano kwa matatu ambapo kwa siku ya jana Bayern waliibuka na ushindi wa goli 3-2 lakini pamoja na ushindi huo haukutosha kuizuiya Barca kuelekea BERLIN ambako ndipo finali hiyo itafanyika mnamo tarehe 6 juni.
"Messi ni mchezaji bora wa muda wote" alisema PEP "Naweza nikamfananisha na PELE na najisikia furaha kumuona katika ubora wake ule ule ambao alikuwa akiuwonyesha akiwa chini yangu" alisema PEP ambae alipata mafanikio wakati MESSI akiwa katika ubora wake kama sasa wakati ambao kocha huyo alikuwa akiinoa Barca kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012 na kufanikiwa kubeba ubingwa wa ulaya mara mbili mwaka 2009 na mwaka 2011

Comments
Post a Comment