KOCHA WA REAL MADRID ASIMAMISHWA MICHEZO MIWILI

Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid abayo iko nyuma kwa alama nne nyuma ya Barca wanaongoza ligi katika msimamo wa ligi kuu ya Hisapania amesimamishwa au kuzuiliwa kuiyongoza timu yake katika michezo miwili katika ligi kuu ya Hispania. Mara baada ya mchezo dhidi ya Vallencia ambao waliambulia suruhu na kuweka pengo la alama nne dhidi vinara wa ligi hiyo Carlo Ancelotti alionekana kupanda hasira na kumvaa refa huku akidai kuwa kachezesha vibaya mchezo huwo na kusababisha kuongeza pengo la pointi katika mbio za kusaka ubingwa wa ligi hiyo. Katika mchezo huo tulishuhudia Ronaldo akikosa mkwaju wa penati na mpaka mwisho matokeo yakawa ni suruhu pacha ya goli 2-2
       Kwa hivyo basi Ancelotti atakosa kuiyongoza timu yake hiyo kwa msimu huu mpaka msimu ujao kwa kuwa idadi ya mechi mbili alizosimamishwa ndizo idadi ya mechi zilizobaki katika ligi kwa hiyo hatokuwepo dhidi ya Espanyol na Getafe
       Barcelona wao wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne huku wakiwa na point 90 na wanatakiwa kushinda mchezo mmoja tu kati ya miwili iliyobaki ili waweze kutawazwa rasmi kama mabingwa wa ligi kuu Hisapania msimu huu amabako wana mchezo dhidi ya Althretico Madrid ugenini na Deportivo na jana kocha wa Barcelona Luic Enrique alionekana kupania kuchukua ndoo ya Laliga mara baada ya kupumzisha majembe ya ili kujiandaa kuiyua ATM.

Comments

Popular posts from this blog

Putting African on Mobile market, through VMK

NIGERIAN SOLDIERS CATCH BOKO HARAM LEARDER ON BORNO.