Messi anaikumbuka hat trick moja tu aliyofunga dhidi ya real Madrid mwaka 2007 na ndio ilikuwa ya kwanza katika maisha yake ya soka

Lionel Messi ameonyesha kuwa na furaha baada ya kuendelea kuifungia team yake na kuwa sehemu ya historia ya klabu yake ya Barcelona nchini Hispania ambapo mpaka sasa ameshavunja na kuweka record kibao
Ambapo mpaka sasa anashikilia record ya kuwa mchezaji aliyetoa pasi nyingi zaid za magoli akiwa juu ya Luis Figo aliyekuwa akiishikiria record hiyo kwa pasi 106 za mwisho katika ligi hiyo ya Spain na amekuwa mshambuliaji mwenye magoli mengi zaidi katka historia ya Laliga lakini bado anaendelea kuwa mfungaji wa kihistoria Barca
Katika mahojiano yaliyokuwa yakiendelea Messi aliulizwa maswali kadhaa yafuatayo

  Mwandishi : unaonekana kuwa na furaha uwapo uwanjani na unapokuwa nje ya uwanja je? Hiyo ni sababu ya wewe kufanya vzuri
   Messi : Kiukweli sikuwa vizuri mwanzoni mwa msimu kwa matatizo na matukio ya nje ya uwanja na ndani ya uwanja lakini pia majeruhi yaliyukuwa yakinisumbua msimu ulioisha kwa hiyo najitahidi niwe pale nnapohitaji kuwa
   Mwandishi : Nikiangalia idadi ya magoli uliyoshinda msimu huu ni 41 kati ya michezo 38 magoli ambayo ni sawa na yale uliyomaliza nayo msimu uliopita je? Hii ni dalili za wewe kurudia ubora wako
   Messi : Kama nlivyojibu awali nilikuwa na majeraha kwa msimu uliopita sikuweza kucheza mechi kadhaa ila kwa sasa najitahidi nifikie malengo kwa kucheza kwa juhudi, tabasamu na nguvu zaidi
   Mwandishi : Kwa msimu huu umekuwa ukisaidiwa na washambuliaji wawili ambao ni Suarez na Neyamar ambapo awali tumekuwa tukiona Messi akishinda na Barca inachukua alama tatu asipofunga Barca mayo inapotea je unajisikiaje kusaidiwa kwa sasa?
    Messi: Kiukweli swala la Mimi kufunga na Barcelona kushinda mchezo hilo silionagi maana Barcelona iko vzuri kila idara na misimu kadhaa Barcelona imekuwa ikiongozwa na washambuliaji wakubwa kwa hiyo kuwepo kwao na mimi ni swala la kazi zaidi
    Mwandishi : Unapendelea kufunga magoli ya aina je ni yale ambayo unafunga nje ya 18 au ni yale unayofunga kwa mipira ya adhabu au yale ya kuwapita walinzi kadhaa na kufunga?
    Messi : Me huwa najali kufunga na sio aina ya goli nlilofunga nipo uwanjani kwa ajili ya kuipa ushindi Barca na sio kufunga aina flani ya magoli
   Mwandishi: Kwa nini imekuwa ni tabia yako pale unapofunga goli tatu ukipewa mpira huwa unahitaji wachezaji wenzako waweke alama zao (sign) kabla hujaondoka nao?
   Messi : Uwanjani sikudaka Mimi sikuzuia peke yangu na kiufupi sikucheza peke yangu nlishilikiana nao ndio maana nkafunga pia kwa hiyo ni heshima kwao kufanya vile
    Mwandishi: Unaiwekaga wapi mipira yako
    Messi: naihifadhi nyumbani ambako huwa naweka tuzo zangu zinginezo
     Mwandishi: Unazikumbuka vipi hat trick ulizowahi kufunga
      Messi: Kiukweli sikumbukia kwa urahisi ila mpaka nnapoangaliaga video au kuhadithiwa na mtu huwa nakumbuka pia
      Mwandishi: Ni hat trick gani ni maalum kwako
      Messi: Ni ile ambayo nlifunga dhidi ya Real Madrid mwaka 2007 ambapo tulitoka suruhu ya goli 3-3 na nlikuwa mfungaji pekee ila si hilo tu ni kwa kuwa ilikuwa ni hat trick yangu ya kwanza na ilikuwa ni dhidi ya real Madrid lakini pia matokeo yale yaliisaidia Barcelona kuongoza ligi
   
Messi
Mwandishi:Ni pongezi zipi unazikumbuka na kuzifurahia pale baada ya kufunga hat trick
Mess: Ni ile ile hat trick dhidi ya Real Madrid nlipokuwa natoka uwanjani Raul alinifuata akanipa pongezi na hii inatokana na jinsi Raul wa kipindi kile alivyokuwa
Mwandishi: Kwa sasa una umri wa miaka 27 hii ni tangu uingie Lamasia ukiwa na umri wa miaka 13 na kwa sasa una mtoto uliyemwita Thiago je kwa sasa Kuna utofauti gani baada ya mazowea ya ubaba?
Messi: Kiukweli niko tofauti na zamani maana endapo Barcelona ikipoteza mchezo nlikuwa siongelei hilo nauchuna mpaka siku nne au tatu zipite ila kwa sasa Thiago kwanza mengine yanafuata na kama tukipoteza mchezo naenda moja kwa moja nyumbani nnapomuona na kucheza nae huwa nakuwa mwepesi wa kupoteza hasira za kupoteza mchezo

NI HAYO TU KWA LEO ILA KWA HABARI ZA KIMICHEZO ZA BARANI ULAYA USIKOSE KUTEMBELEA UKURASA HUU WA www.swahilimagazinetz.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Putting African on Mobile market, through VMK

NIGERIAN SOLDIERS CATCH BOKO HARAM LEARDER ON BORNO.