Man_city waangukia pua kuivaa Man U jumapili

 Manchester city ilipoteza mechezo wake wa jana ambao laiti kama wangeshinda basi wangerudi katika nafasi yao ya pili na kumshusha Arsenal anaeikalia nafasi hiyo kwa point 63 wakiwa nyuma ya Chelsea wenye alama 70 huku wakiwa na kipolo cha mchezo mmoja mkononi na mpaka sasa imecheza michezo 30 ya ligi
Manchester city mpaka sasa wamepoteza michezo mitatu kati ya mitano waliocheza mfululizo ukiwemo ule mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya waliofungwa na Barcelona
 manchester city wako katika wakati mgumu baada ya kupoteza mchezo wa jana wameendelea kusalia katika nafasi yao ya nne nyuma ya watani wao wa jadi Manchester united kwa tofauti ya pointi moja, mara baada ya kupoteza mchezo wa jana kumekuwa na wasiwasi wa kushindwa kuwania nafasi nne za juu endapo wataendelea na kiwango duni walichokionyesha kwenye mchezo wa jana dhidi ya Crystal parace ingawa walionyesha kupoteza nafasi kadhaa lakini ule umakini wa Aguero umeonekana kupungua akiwa anafanya kazi ya kulenga miamba badala ya nyavu ila Yaya Toure ndiye alionyesha juhudi za kuibeba City baada ya kuifungia goli la kufutia machozi mnamo dakika ya 78' na magoli ya Crystal parace yalifungwa na G. Murray mnamo dakika ya 34' ya mchezo goli ambalo ni wazi ilikuwa ni la kuotea. Parace hawakuishia hapo waliongeza goli mnamo dakika ya 48' kupitia kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa umaridadi wa hali ya juu kupitia kwa J. Puncheon amabae alimpoteza J. Hart na mchezo ukamalizika kwa ushindi kwa Parace wa goli 2 - 1 na kuwaacha wachezaji wa Man City wakiwa wamechoka bila kutarajia kilichowakuta
Tarehe 12 April jumapili hii wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya mahasimu wao wa pale OT ambao wanaonekana kuimarika wakiwa wameshinda mfululizo katika moja ya michezo yao mitatu migumu dhidi ya Spurs, Liverpool na Aston Villa
Kwa upande wa Manchester city wanatakiwa kushinda mchezo huu mgumu ili waweze kusogea walau hadi nafasi ya tatu na endapo kama Arsenal atapoteza mchezo wake dhidi ya Burnley wanaopigana wasishuke daraja wakiwa katika nafasi ya 18 na alama 26 mkononi mchezo utachezwa siku ya jumamosi

Comments

Popular posts from this blog

Bad news for Manchester United Manchester City and Arsenal in UEFA Champions League

State’s financial support to farming reaches 1tri/-