ORODHA YA MABEKI 10 BORA ULAYA NA STORY KUHUSU AIBU YA DAVID LUIZ KUGEUZWA KUWA MNARA WENYE UWAZI KWA CHINI
Jana tuliishuhudia Barcelona ikiichabanga bila huruma PSG waliokuwa wenyeji katika mechi ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambako tulishuhudia Barca ikiibuka na ushindi wa goli 3-1 ushindi ambao ulinogeshwa na matobo ya Luis Suarez akimpiga David Luiz ambapo moja kati ya hayo yalizaa goli kitu ambacho kimeiyumiza PSG kwa usajili waliofanya kwa beki huyo ambao uliwakost pound mil 50 na kushuhudia wakiangukia pua Jana
Lakini kwa upande wangu nilishawahi kusema kuwa David Luiz bila uwepo wa Thiago Silva ni sawa na mlango mtupu wenye pazia tu maana uwepo wa Thiago Silva humpa amasa Luiz ambae hucheza akifuata maelekezo mengi na kampani ya kutosha kutoka kwa rafiki yake au kaka yake wenye uraia wa nchi moja. Jana tukamshuhudia Luiz akifanywa kama mtoto na bwana Luis Suarez
ANGALIA ORODHA YA WALINZI MAKINI DUNIANI
10. Raphael Verane
09. Andrea Barzagli
08. Ezequiel Garay
07. Gerard Pique
06. Dante
05. Sergio Ramos
04. Giorgio Chiellini
03. Vincent Kompany
02. Mats Hammels
01. Thiago Silva
Hao walionekana kuwa bora na tunamuona Thiago Silva akishika usukani....
KWA STORY NYINGI ZA SOKA LA ULAYA USIWE MVIVU KUTEMBELEA www.swahilimagazinetz.blogspot.com
Comments
Post a Comment