EPL yawaka moto Ronaldo akunja ngumi

 Katika wiki kadhaa ligi nyingi ulaya zilikuwa zimesimama na badala yake kulikuwa na mashindano katika timu za taifa na pia ni mechi za kirafiki
Lakini kutokana na kiu ya muda mrefu kwa mashabiki wa ligi za ulaya sasa ilirejea katika mwisho wa juma lilopita
Jumamosi kulikuwa na baadhi ya mechi kali zilizokutanisha timu kadhaa kubwa ambako moja kati ya mechi kali iliyokuwa ikisubiriwa na wengi ni mechi baina ya Arsenal na Liverpool mechi ambayo arsenal walikuwa nyumbani emirates ambako jumamosi hiyo walijichinjia jogoo lao la pasaka na kuliweka kwenye jokofu kwa ajili ya pasaka, Arsenal iliicharaza Liverpool kwa idadi ya magoli 4 kwa 1 ambapo magoli hayo yalifungwa na Bellerin dakika ya 37 akipokea pasi safi kutoka kwa Ramsey na dakika ya 40 ya mchezo mjerumani M. Ozil alipiga faulo safi aliyozama wavuni ambayo bila shaka ni faulo bora tangu aanze kukipga arsenal na Ramsey hakuchoka kutengeneza magoli alimkatia pande maridadi Sanchez ambae alipiga muwa uliozama wavuni na kuandika bao la tatu katika dakika ya 45 na kwa kipind cha kwanza tokeo likawa hivyo yaani tatu kwa nunge. Kipindi cha pili Liverpool walionyesha adabu ya soka ili kuzuia kipigo cha aibu na walipata goli kwa kupitia mkwaju wa penalty dakika ya 76 ambayo ilizaa goli lililofungwa na J. Henderson kwa mkwaju mzur wa penalty dakika tisini za mchezo ziliisha huku Arsenal ikiongoza kwa goli tatu kwa moja lakini ingekuwa ajabu kama Olivier Giroud asingefunga maana anaonekana kutaka kuweka heshima baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Sanchez alizamisha wavuni mpira huo na kuandika bao la nne katika dakika ya kwanza ya nyiongeza ya mchezo huo
Manchester United pia iliamua kukaa katika nafasi ya tatu kwa kishindo baada ya kuicharaza Aston Villa kwa mabao matatu kwa moja mabao yaliyofungwa na Herrera aliyefunga mawili na jingine kufungwa na Rooney akimalizia assist safi kutoka kwa Di maria na goli pekee la Villa liliwekwa wavuni na Benteke akimalizia mpira uliopigwa na A. Cole
Kwa upande wangu nlibahatika kushuhudia goli kali wakati wa mech kati ya Chelsea na Stock city ambayo ilimalizika kwa ushind kwa Chelsea wa goli mbili kwa moja magoli yaliofungwa na Hazard na Luic Remy na goli la maajabu kabisa kwa upande wa Stock lilifungwa na C. Adam aliemchungulia kipa na kuachia mkwaju kutoka nyuma ya duara la kati ya uwanja na kumshuhudia kipa Chelsea akipata mateso kuudaka maana alikuwa katokea miguu kadhaa

Lakini pia binafsi nlikuwa nkifatilia mchezo wa West bromwich dhidi ya QPR ambao ulimalizika kwa ushindi wa goli nne kwa moja kwa QPR ambapo nlimuona Chalie Austin mshambuliaji anaejitahidi kuinusuru QPR isishuke daraja akitoa assist moja na kufunga goli moja. Mshambuliaji huyu ameonekana akishindana na kina Costa, Kane na Agüero katika kutwa kiatu cha ufungaji bora wa ligi ya EPL  ambapo mpaka sasa orodha hiyo inaongozwa na Kane na Costa wote wakiwa na magoli 19 wakifuatiwa na Agüero mwenye magoli 17 huku Chalie Austin akiwatafuta kimya kimya kwa magoli yake 16, kiukweli huyu jamaa anakipaji cha pekee kushindana na wanne waliojuu yake ambao wanazungukwa na kuchezeshwa na wachezaji wazuri zaidi ya wale wanaopatikana QPR inayohangaika isishuke daraja na nategemea makubwa zaidi kwa Austin endapo akizungukwa na watu kama kina Febrigas
Nchini uhispania tuliona mchezo wa mpira wa Pete ambao ulikuwa ni baina ya Real Madrid na Granada ambao uliisha kwa magoli Tisa kwa moja ushindi ambao uliimarishwa na urejeo wa James Rodriguez aliyekuwa majeruhi lakini cha ajabu zaidi ni pale Ronaldo alipoudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ni bora zaid ambako hapo awali zilitoka takwimu za mshambuliaji bora zaidi huku yeye akishika nafasi ya 29
Ronaldo alitupia tano ishara ya kukunja ngumi kwa mara yake ya kwanza katika career yake na kuwaacha wengi na mishangao wakihoji imekuwaje lakini kwa haraka nkamuona Rodriguez akichukua nafasi kubwa katika ushindi huo mnono na Modric akiwa moto wa kuotea mbali na kwa upande wa wapinzani wao Barcelona walipata point tatu kwa mbinde baada ya kushinda goli moja kupitia kwa beki wake wa kati Jeremi Methew

Comments

Popular posts from this blog

Putting African on Mobile market, through VMK

NIGERIAN SOLDIERS CATCH BOKO HARAM LEARDER ON BORNO.